Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Serikali ya kaunti

Jinsi serikali ya kaunti inavyofanya kazi

Kenya ina kaunti 47, kila moja na serikali yake karibu na wananchi. Ona kazi za kaunti, nani anaziongoza, na jinsi unavyoweza kushiriki.

Ugatuzi ni nini?

Ugatuzi ni kugawana mamlaka kati ya serikali ya kitaifa na serikali 47 za kaunti, ili maamuzi yafanywe karibu na wananchi.

Art. 6

(1) Eneo la Kenya limegawanywa katika kaunti zilizotajwa katika Mpangilio wa Kwanza. (2) Serikali katika viwango vya kitaifa na kaunti ni tofauti na zinategemeana na Zitaendesha mahusiano yao ya uelewanaji kwa misingi ya mashauriano na ushirikiano. (3) Asasi ya Serikali ya kitaifa itahakikisha ufikiaji wa huduma zake bora katika sehemu zote za Jamhuri kwa njia inayofaa na kulingana na hali ya huduma inayotakikana

Soma kifungu kamili →
Art. 174

Malengo ya Serikali ya ugatuzi ni- (a) kuhakikisha kuwa kuna mamlaka ya kidemokrasia na uwajibikiaji wa Serikali ; (b) kuhimiza umoja wa kitaifa kwa kutambua uanuwai wa jamii mbalimbali; (c) kuwapa watu katika kila ngazi mamlaka ya kujitawala na kushiriki katika matumizi ya mamlaka ya Serikali katika kufanya maamuzi ya mambo yanyowaathiri; (d) kutambua haki za jamii zote katika kusimamia masuala ya jamii zao na kujiendeleza zaidi; (e) kulinda na kuhamasisha maslahi na haki za jamii za watu walio wachache na zile za watu waliotengwa; (f) kustawisha miradi ya kijamii na kiuchumi na utoaji wa huduma za karibu na zilizo rahisi ili kumfikia kila mtu nchini Kenya; (g) kuhakikisha kuna ugavi sawa wa rasilmali zote za kijamii na za kitaifa kote nchini. (h) kufanikisha ugatuzi wa mamlaka ya taasisi za Serikali, uendeshaji wake wa shughuli ama huduma kutoka mji mkuu wa Kenya; na (i) kuhakikisha kuna kudhibiti na kugawana mamlaka kwa njia iliyo sawa.

Soma kifungu kamili →

Kaunti 47

Katiba inagawanya Kenya katika kaunti 47. Kila kaunti ina serikali yake.

Sehemu mbili za kaunti

Kila kaunti ina utendaji unaoendesha huduma, na bunge linalotunga sheria na kukagua fedha.

Utendaji wa Kaunti

Gavana, Naibu wa Gavana na Kamati ya Utendaji ya Kaunti huendesha huduma za kaunti na kutekeleza sheria za kaunti.

Art. 176

(1) Kila kaunti itakuwa na Serikali yake itakayokuwa na bunge na Baraza la Kaunti. (2) Kila Serikali ya kaunti itagatua shughuli zake na utoaji wa huduma ili kuhakikisha kwamba imepata ufanisi wa kutekeleza majukumu yake kadiri iwezekanavyo.

Soma kifungu kamili →
Art. 179

(1) Mamlaka kuu ya kaunti yamepewa, na yatatekelezwa, na kamati za mamlaka kuu za Kaunti. (2) Kamati ya mamlaka kuu ya Kaunti inajumuisha- (a) gavana wa kaunti na naibu wake; na (b) wanachama walioteuliwa na gavana wa kaunti, kwa idhini ya baraza, kutoka kwa watu wasio wanachama wa baraza. (3) Idadi ya wanachama walioteuliwa kwa mujibu wa ibara ya (2)(b) haitazidi: (a) thuluthi moja ya wanachama wa bunge la kaunti kama bunge hilo halina zaidi ya wanachama zaidi ya thelathini; au (b) kumi; kama baraza lina wanachama thelathini au zaidi. (4) gavana wa kaunti na naibu wake, watakuwa afisa mkuu na naibu wa afisa mkuu wa kaunti, mtawalia. (5) Gavana wa kaunti asipokuwepo, naibu wake ana mamlaka ya kutosha ya kuendesha shughuli zote na majukumu ya gavana wa kaunti. (6) Wanachama wa kamati kuu ya kaunti wanawajibikia gavana wa kaunti katika utekelezaji wa majukumu na mamlaka yao. (7) Iwapo afisi ya gavana itakuwa wazi, wanachama wa mamlaka kuu ya kaunti walioteuliwa chini ya ibara ya (2) (b) watakuwa hawana kazi.

Soma kifungu kamili →
Art. 183

(1) Kamati kuu ya kaunti ina majukumu yafuatayo: (a) utekelezaji wa sheria za bunge la kaunti; (b) utekelezaji, katika kaunti , sheria za taifa inavyohitajika kisheria; (c) kusimamia shughuli za utawala wa kaunti na idara zake; na (d) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Katiba hii na sheria ya nchi. (2) kamati kuu ya kaunti inaweza kuandaa sheria iliyopendekezwa na kuziwasilisha kwa bunge la kaunti. (3) kamati kuu ya kaunti itatoa ripoti kamili za mara kwa mara kwa baraza la kaunti kuhusu masuala yaliyo chini ya udhibiti wa kamati hiyo.

Soma kifungu kamili →

Bunge la Kaunti

Wajumbe wa Bunge la Kaunti (MCAs) wanaochaguliwa kutoka wadi, wakiongozwa na Spika, hutunga sheria za kaunti na kuidhinisha bajeti ya kaunti.

Art. 177

(1) Baraza la kaunti lina wanachama wafuatao- (a) wanachama waliochaguliwa na wapiga kura waliosajiliwa katika wadi, kila wadi ikijumuisha eneo moja la uwakilishi siku ile ya kupiga kura ya uchaguzi mkuu wa kuwachagua wabunge, itakayokuwa Jumanne ya pili ya mwezi Agosti baada ya kila miaka mitano (b) idadi ya wabunge maalum ili kuhakikisha kuwa hakuna zaidi ya wabunge thuluthi mbili wa jinsia moja katika bunge hilo. (c) idadi ya wanachama kutoka katika makundi yaliyotengwa, wakiwemo watu walemavu, jamii za watu wachache na vijana, kama inavyopendekezwa katika Sheria ya Bunge; na (d) spika, asiye mwanachama rasmi. (2) Wanachama wanaotajwa katika ibara ya (1) (b) na (c) watatateuliwa na vyama vya kisiasa kwa mgao wa kutegemea idadi ya viti chama cha kisiasa kilivyopata katika uchaguzi huo, katika kaunti hiyo chini ya Ibara ya (a) kulingana na kifungu cha 90. (3) Kujaza viti maalum kwa mujibu wa ibara ya (1) (b) kutaamuliwa baada ya kutangazwa kwa wanachama waliochaguliwa katika kila wadi. (4) Baraza la kaunti huchaguliwa kwa kipindi cha miaka mitano.

Soma kifungu kamili →
Art. 185

(1) Mamlaka ya kutunga sheria ya kaunti yamepatiwa na yatatekelezwa na baraza la kaunti. (2) Baraza la kaunti, linaweza kutunga sheria zozote muhimu, zinazoshughulikia masuala yanayohusiana na, ufanikishaji wa mamlaka na majukumu yake, na utekelezaji wa mamlaka ya serikali ya kaunti kwa mujibu wa Mpangilio wa nne. (3) Baraza la kaunti, likizingatia kanuni ya kugawana mamlaka, lina uwezo wa kusimamia kamati ya mamlaka kuu ya kaunti na idara nyingine za mamlaka katika kaunti. (4) Baraza la kaunti laweza kupokea na kuidhinisha mipango na sera kwa- (a) usimamizi na utumiaji wa rasilmali za kaunti; na (b) kustawisha na kusimamia miundomsingi na idara zao.

Soma kifungu kamili →

Kazi za kaunti

Huduma za ndani zilizoorodheshwa katika Ratiba ya Nne ya Katiba.

  • Vituo vya afya na zahanati za ndani.
  • Barabara za ndani na taa za mitaa.
  • Masoko na biashara.
  • Maji na usafi wa mazingira.
  • Kilimo na mashamba ya ndani.
  • Elimu ya awali ya watoto.
Art. 186

(1 ) Isipokuwa kama ilivyotajwa katika Katiba hii, mamlaka na majukumu ya Serikali ya taifa na zile za kaunti, mtawalia,ni kama yalivyoelezwa katika Mpangilio wa Nne (2) Jukumu linalopatikana katika zaidi ya ngazi moja ya Serikali ni jukumu lililo katika eneo zaidi ya moja la utawala la ngazi hizo za Serikali. (3) Jukumu ambalo halijatolewa na Katiba hii au na sheria ya taifa kwa kaunti, ni jukumu ya Serikali ya taifa. (4) Kuwa yakini zaidi, bunge litatunga sheria ya Jamhuri katika suala lolote.

Soma kifungu kamili →

Jinsi kaunti inavyopata fedha

Kaunti lazima iwe na fedha za kutoa huduma.

Mgao wa haki

Kaunti hupata mgao wa haki wa mapato ya kitaifa, unaoamuliwa kila mwaka.

Art. 202

(1) Mapato yanayozalishwa katika kiwango cha kitaifa yatagawanywa sawa kwa serikali ya kitaifa na serikali za kaunti; (2) Serikali za kaunti zinaweza kupewa mgao wa ziada kutoka kwa sehemu ya mapato ya serikali ya kitaifa, kwa masharti au bila masharti.

Soma kifungu kamili →
Art. 203

(1) Vigezo vifuatavyo vitatumiwa kutoa uamuzi kuhusu mgao sawa uliotajwa katika kifungu cha 202 na katika sheria zote za kitaifa kuhusu serikali za kaunti kama zilivyotungwa kwa mujibu wa masharti ya sura hii – (a) masilahi ya kitaifa; (b) kifungu kingine ambacho kinahitajika kwa mujibu wa deni la umma na mahitaji mengine ya kitaifa; (c) mahitaji ya serikali ya kitaifa yatakayoamuliwa kwa misingi ya kigezo cha kutopendelea; (d) haja ya kuhakikisha kuwa serikali za kaunti zina uwezo wa kutekeleza majukumu zilizopewa; (e) uwezo wa kifedha na ufanisi wa serikali za kaunti; (f) maendeleo na mahitaji mengine ya serikali za kaunti; (g) tofauti za kiuchumi miongoni na kati ya kaunti na sababu ya kutatua matatizo hayo; (h) haja ya kuchukua hatua kwa mujibu wa maeneo na makundi yaliyotengwa; (i) haja ya kuboresha uchumi kwenye kila kaunti na kutoa motisha kwa kila kaunti kuboresha uwezo wake wa kuzalisha mapato; (j) kutamani mgao wa mapato ulio thabiti na unaoweza kutabirika; na (k) haja ya wepesi katika kukabiliana na majanga na mahitaji mengine ya muda katika misingi ya kigezo cha kutopendelea. (2) Kwa kila mwaka wa fedha, mgao unaolingana wa mapato yanayozalishwa na taifa ambayo yatagawiwa serikali za kaunti hayatapungua asilimia kumi na tano ya mapato yote ambayo serikali ya kitaifa inayozalisha. (3) Jumla ya fedha zilizotajwa katika Ibara ya (2) zitapigwa hesabu katika misingi ya ukaguzi wa juzi zaidi wa hesabu ya mapato yaliyokusanywa, kama itakavyoidhinishwa na Baraza la Kitaifa.

Soma kifungu kamili →

Mfuko wa Mapato wa Kaunti

Fedha za kaunti huingia katika Mfuko wa Mapato wa Kaunti.

Art. 207

(1) Hazina ya Mapato ya kila serikali ya Kaunti imeundwa. Hazina hii italipwa pesa zote zilizozalishwa au kupokelewa na, au kwa niaba ya serikali ya kaunti, isipokuwa fedha ambazo kwa sababu maalum zimetengwa na Sheria ya Bunge. (2) Fedha zinaweza kutolewa kutoka kwa Hazina ya Mapato ya serikali ya Kaunti kwa ajili :- (a) Kama malipo dhidi ya Hazina ya Mapato ambayo yamekubaliwa na Sheria ya Bunge au sheria za serikali hiyo ya kaunti; au (b) kama ilivyoidhinishwa na sheria ya matumizi ya fedha katika serikali hiyo ya kaunti. (3) Fedha hazitatolewa kwa Hazina ya Mapato mpaka Msimamizi wa Bajeti atakapoidhinisha. (4) Sheria ya Bunge inaweza – (a) kutoa idhini zaidi ya kutoa fedha kutoka kwa Hazina ya Mapato ya Serikali ya Kaunti. (b) kuruhusu serikali za kaunti kuanzisha hazina nyingine za mapato na usimamizi wa hazina kama hizo.

Soma kifungu kamili →

Mapato ya ndani

Kaunti inaweza pia kukusanya ada na malipo ya ndani.

Art. 209

(1) Ni serikali ya kitaifa pekee ambayo imepewa uwezo wa kutoza- (a) kodi ya mapato; (b) ushuru wa thamani; (c) ushuru wa forodha na kodi nyingine katika bidhaa zinazoingizwa na kuuzwa nje ya nchi.; na (d) mapato ya ushuru. (2) Sheria ya Bunge inaweza kuipa mamlaka serikali ya kitaifa kutoza ushuru au kodi nyingine yoyote, isipokuwa ushuru uliotajwa katika ibara ya (3) (a) na (b). (3) Serikali ya kaunti inaweza kutoza:- (a) ushuru kwa mali; (b) kodi za burudani; na (c) na kodi nyingine yoyote ambayo imeruhusiwa na Sheria ya Bunge. (4) Serikali ya kitaifa na serikali za kaunti zinaweza kutoza ushuru wa huduma. (5) Utozaji ushuru na mamlaka mengine ya kuzalisha mapato ya serikali ya kaunti hautafanywa kwa njia ambayo inakiuka sera za kiuchumi za kitaifa, shughuli za kiuchumi zinazotekelezwa ndani ya mipaka ya kaunti au uzungushwaji wa bidhaa katika nchi nzima, huduma, mtaji au ajira.

Soma kifungu kamili →

Ruzuku maalum

Wakati mwingine serikali ya kitaifa hutoa fedha za ziada kwa miradi maalum.

Art. 202

(1) Mapato yanayozalishwa katika kiwango cha kitaifa yatagawanywa sawa kwa serikali ya kitaifa na serikali za kaunti; (2) Serikali za kaunti zinaweza kupewa mgao wa ziada kutoka kwa sehemu ya mapato ya serikali ya kitaifa, kwa masharti au bila masharti.

Soma kifungu kamili →

Jinsi unavyoshiriki

Serikali ya kaunti iko karibu zaidi na maisha yako ya kila siku — hivyo sauti yako ni muhimu.

Ushiriki wa umma

Mabunge ya kaunti lazima yaruhusu umma kutoa maoni kabla ya maamuzi muhimu.

Art. 196

(1) Baraza la kaunti – (a) litaendesha shughuli zake kwa uwazi, na kufanya vikao vyake na vile vya kamati zake mbele ya umma; na (b) kuhimiza watu kushiriki katika kutunga sheria na katikacshughuli nyingine za baraza na kamati zake. (2) Baraza la kaunti halitawaacha nje watu, au vyombo vya habari, katika kikao chochote ila katika hali ambapo spika wa bunge ametoa uamuzi na sababu za kutosha za kufanya hivyo. (3) Baraza litatunga sheria itakayoonyesha mamlaka, haki, na kinga ya mabaraza ya kaunti, jamii na wanachama wake.

Soma kifungu kamili →

Wasiliana na viongozi wako

Zungumza na Gavana au MCA wako kuhusu mahitaji ya wadi yako.

Maombi

Wasilisha ombi kwa bunge la kaunti kuhusu suala linalokuhusu.

Art. 196

(1) Baraza la kaunti – (a) litaendesha shughuli zake kwa uwazi, na kufanya vikao vyake na vile vya kamati zake mbele ya umma; na (b) kuhimiza watu kushiriki katika kutunga sheria na katikacshughuli nyingine za baraza na kamati zake. (2) Baraza la kaunti halitawaacha nje watu, au vyombo vya habari, katika kikao chochote ila katika hali ambapo spika wa bunge ametoa uamuzi na sababu za kutosha za kufanya hivyo. (3) Baraza litatunga sheria itakayoonyesha mamlaka, haki, na kinga ya mabaraza ya kaunti, jamii na wanachama wake.

Soma kifungu kamili →

Fuatilia bajeti

Uliza jinsi fedha za kaunti zinavyopangwa na kutumika.

Art. 201

Kanuni zifuatazo zitaongoza Vifungu vyote vya fedha za umma katika taifa:- (a) Kutakuwa na uwazi na uwajibikaji, ikiwa ni pamoja na kuhusika kwa umma katika masuala ya kifedha. (a) Mfumo wa fedha za umma utakuza jamii yenye usawa, hasa:- (i) Mzigo wa utozaji ushuru utasawazishwa;. (ii) Mapato yanayopatikana katika kiwango cha kitaifa yatagawanywa sawa kati ya serikali ya kitaifa na serikali za kaunti;. (iii) Matumizi yatachangia usawazishaji wa kimaendeleo nchini, ikiwa ni pamoja na mgao maalum kwa makundi ya watu kutoka maeneo yaliyotengwa; na (b) Mizigo na faida za matumizi ya mapato na ukopaji wa umma itagawanywa sawa kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo; (c) fedha za umma lazima zitumiwe kwa busara na uwajibikaji; na (d) Usimamizi wa fedha lazima uwajibikiwe vyema na ripoti ya hazina ya serikali iwe wazi.

Soma kifungu kamili →

Nani anafanya nini katika kaunti

GavanaHuongoza kaunti na kutekeleza sheria za kaunti.
Naibu wa GavanaHumsaidia Gavana.
Kamati ya Utendaji ya KauntiHuendesha idara na huduma za kaunti.
Bunge la KauntiHutunga sheria za kaunti, huidhinisha bajeti na husimamia.
MCAsHuwakilisha wadi na kuinua masuala ya ndani.
Serikali ya kitaifaHuweka sera za kitaifa na kusaidia kaunti.

Soma vifungu halisi

Kila hoja kwenye ukurasa huu inatoka katika Katiba. Gusa rejeo kuona kifungu halisi.

    Tafuta →