Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Uchaguzi

Jinsi uchaguzi unavyofanya kazi nchini Kenya

Kuanzia kujiandikisha kupiga kura hadi matokeo ya mwisho: fuata hatua, mtambue IEBC, na uone jinsi kura yako inavyokuwa sauti yako.

Kura yako ni nguvu yako

Uchaguzi ni jinsi wananchi wanavyowapa viongozi mamlaka — na jinsi wanavyoyarudisha. Kila mwananchi mzima ana haki ya kupiga kura na kugombea.

Art. 1(1)

(1) Mamlaka yote makuu ni ya wananchi wa Kenya na yanaweza kutekelezwa tu kulingana na Katiba hii.

Soma kifungu kamili →
Art. 38

(1) Kila mwananchi ana uhuru wa kuwa na uchaguzi wa kisiasa, ikiwemo haki ya – (a) kuunda, au kushiriki katika uundaji wa chama cha kisiasa; (b) kushiriki katika shughuli za, au kusajili wanachama kwa niaba ya chama cha kisiasa; au (c) kufanyia kampeni chama cha kisiasa. (2) Kila mwananchi ana haki ya kushiriki katika uchaguzi huru, wa haki na unaofanyika mara kwa mara kwa misingi ya haki ya kupiga kura kwa wote na uhuru wa hiari ya mpiga kura kwa - (a) shirika au afisi yoyote ya umma iliyobuniwa chini ya Katiba hii na inayofanya uchaguzi; na (b) kiongozi wa afisi yoyote ya chama cha kisiasa ambacho mwananchi huyo ni mwanachama. (3) Kila raia akiwa mtu mzima ana haki pasipo na masharti yasiyo na busara,- (a) kujiandikisha kama mpiga kura; (b) kupiga kura ya siri katika uchaguzi wowote au katika kura ya maamuzi; na (c) kugombea wadhifa katika afisi ya umma, au afisi katika chama cha kisiasa ambacho yeye ni mwanachama na endapo atachaguliwa, ashike usukani.

Soma kifungu kamili →

Viongozi sita unaowachagua

Katika uchaguzi mkuu, unaofanyika kila miaka mitano, unapiga kura kwa nafasi sita.

Rais

Huongoza serikali ya kitaifa.

Art. 136

(1) Rais atachaguliwa na wapigakura waliosajiliwa katika uchaguzi wa kitaifa utakaoendeshwa kwa mujibu wa Katiba hii na Sheria nyingine yoyote ya Bunge inayothibiti uchaguzi wa Rais. (2) Uchaguzi wa Rais utafanyika- (a) siku moja na ile ya uchaguzi mkuu wa Wabunge, ikiwa ni siku ya Jumanne ya pili ya mwezi Agosti ya kila mwaka wa tano; au (b) katika hali ambazo zinatajwa kwenye ibara ya 146.

Soma kifungu kamili →

Gavana

Huongoza serikali ya kaunti yako.

Art. 180

(1) Gavana wa kaunti atachaguliwa moja kwa moja na wapiga kura waliosajiliwa katika kaunti hiyo, siku ile ya uchaguzi mkuu wa wabunge, itakayokuwa Jumanne ya pili ya mwezi Agosti, baada ya kila miaka mitano. (2) Kuhitimu kuchaguliwa kuwa gavana wa kaunti, mtu lazima awe amehitimu kuchaguliwa kuwa mwanachama katika baraza la kaunti. (3) Ikiwa mgombea kiti cha gavana mmoja tu atateuliwa, mtu huyu atatangazwa kuwa amechaguliwa. (4) Ikiwa wagombea kiti cha gavana wawili au zaidi watateuliwa, kura zitapigwa katika kaunti hiyo na mgombeaji atakayepata kura nyingi zaidi atatangazwa kuwa mshindi. (5) Kila mgombea kiti cha gavana wa kaunti atamteua mtu mmoja ambaye amehitimu kuchaguliwa kama gavana wa kaunti kuwa mgombea kiti cha naibu gavana. (6) Mtu hatahudumu afisini- (a) kama gavana wa kaunti kwa vipindi zaidi ya viwili; au (b) kama naibu gavana kwa vipindi zaidi ya viwili. (7) Kwa mujibu wa ibara ya (7), mtu ambaye hajaingia afisi ya gavana wa kaunti atachukuliwa kuwa amehudumu kwa kipindi kizima, kwa mujibu wa kifungu cha 182 (3) (b).

Soma kifungu kamili →

Seneta

Huwakilisha kaunti yako katika Seneti.

Art. 98

(1) Seneti itajumuisha- (a) wanachama arobaini na saba, kila mmoja wao akiwa amechaguliwa na wapigakura waliosajiliwa kwenye kaunti, na kila kaunti ikiwa ni eneowakilishi la mwanachama mmoja; (b) wanachama wanawake kumi na sita watakaoteuliwa na vyama vya kisiasa kulingana na usawa wao wa wanachama kwenye Seneti waliochaguliwa chini ya ibara ya (a) kwa mujibu wa Kifungu cha 90; (c) wanachama wawili wakiwa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja ili kuwakilisha vijana; (d) wanachama wawili wakiwa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja wakiwakilisha watu wenye ulemavu; na (e) Spika atakayekuwa mwanachama m’badala kwa mujibu wa wadhifa wake. (2) Wanachama waliotajwa katika ibara ya (1) (c) na (d) watachaguliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 90. (3) Hakuna chochote katika Kifungu hiki kitafasiriwa kama kinachomuondoa mtu yeyote katika ugombeaji wa uchaguzi chini ya ibara ya (1) (a).

Soma kifungu kamili →

Mwakilishi wa Wanawake

Huwakilisha kaunti yako, na kutetea maslahi ya wanawake, katika Bunge la Kitaifa.

Art. 97

(1) Baraza la Kitaifa litajumuisha – (a) wanachama mia mbili tisini waliochaguliwa na wapigakura, kila mmoja wao akiwa amechaguliwa na wapigakura waliosajiliwa kwa eneobunge moja lililo mwanachama; (b) wanawake arobaini na saba, kila mmoja wao akiwa amachaguliwa na wapigakura waliosajiliwa kwenye kaunti, kila kaunti ikihusisha mwanachama mmoja wa eneobunge; (c) wanachama kumi na wawili walioteuliwa na vyama vya kisiasa vya bunge kulingana na usawa wa wanachama wa Baraza la Kitaifa kwa mujibu wa Kifungu cha 90, kuwakilisha maslahi ya watu maalumu ikiwa ni pamoja na vijana, watu wenye ulemavu na wafanyakazi; na (d) Spika, ambaye ni mwanachama m’badala . (2) Hakuna kifungu chochote katika Kifungu hiki kinachoweza kufasiriwa kama kumuondoa mtu yeyote katika ugombea uchaguzi chini ya ibara ya (1) (a).

Soma kifungu kamili →

Mbunge (MP)

Huwakilisha eneobunge lako katika Bunge la Kitaifa.

Art. 101

(1) Uchaguzi mkuu wa wabunge utafanyika Jumanne ya pili ya mwezi wa Agosti katika kila mwaka wa tano. (2) panapotokea nafasi katika afisi ya mbunge wa Baraza la Kitaifa, lililotajwa chini ya Kifungu cha 97 (1) (c), au katika Seneti chini ya Kifungu cha 98 (1) (b), (c) ama (d), Spika mhusika, katika kipindi cha siku ishirini na moja za kutokea nafasi hiyo ya kazi, atatoa notisi kwa maandishi kuhusu nafasi hiyo ya kazi kwa- (a) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka; na (b) chama cha kisiasa ambacho kupitia kwa orodha yake ya chama ndipo mwanachama huyo alipokuwa amechaguliwa au kuteuliwa. (3) Nafasi hiyo iliyotajwa katika Ibara ya (2) kwa, kuambatana na Ibara ya (5), itajazwa kwa namna iliyoagizwa na Sheria ya Bunge ndani ya muda wa siku ishirini na moja baada ya kutangazwa na Spika mhusika. (4) Panapotokea nafasi ya kazi katika afisi ya mwanachama wa Baraza la Kitaifa aliyechaguliwa chini ya Kifungu cha 97 (1) (a) au (b), au wa Seneti aliyechaguliwa chini ya Kifungu cha 98 (1) (a)- (a) Spika mhusika, kwa muda wa siku ishirini na moja baada ya kutokea kwa nafasi hii, atatoa notisi kuhusu nafasi hii kwa kuiandikia Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka; na (b) uchaguzi mdogo utafanyika katika muda wa siku tisini baada ya kutokea kwa nafasi hiyo ya kazi, kuambatana na ibara ya (5). (5) Nafasi iliyotajwa katika ibara ya (4) haitajazwa katika kipindi cha miezi mitatu inayotangulia uchaguzi mkuu.

Soma kifungu kamili →

Mjumbe wa Bunge la Kaunti (MCA)

Huwakilisha wadi yako katika bunge la kaunti.

Art. 177

(1) Baraza la kaunti lina wanachama wafuatao- (a) wanachama waliochaguliwa na wapiga kura waliosajiliwa katika wadi, kila wadi ikijumuisha eneo moja la uwakilishi siku ile ya kupiga kura ya uchaguzi mkuu wa kuwachagua wabunge, itakayokuwa Jumanne ya pili ya mwezi Agosti baada ya kila miaka mitano (b) idadi ya wabunge maalum ili kuhakikisha kuwa hakuna zaidi ya wabunge thuluthi mbili wa jinsia moja katika bunge hilo. (c) idadi ya wanachama kutoka katika makundi yaliyotengwa, wakiwemo watu walemavu, jamii za watu wachache na vijana, kama inavyopendekezwa katika Sheria ya Bunge; na (d) spika, asiye mwanachama rasmi. (2) Wanachama wanaotajwa katika ibara ya (1) (b) na (c) watatateuliwa na vyama vya kisiasa kwa mgao wa kutegemea idadi ya viti chama cha kisiasa kilivyopata katika uchaguzi huo, katika kaunti hiyo chini ya Ibara ya (a) kulingana na kifungu cha 90. (3) Kujaza viti maalum kwa mujibu wa ibara ya (1) (b) kutaamuliwa baada ya kutangazwa kwa wanachama waliochaguliwa katika kila wadi. (4) Baraza la kaunti huchaguliwa kwa kipindi cha miaka mitano.

Soma kifungu kamili →

Nani anaendesha uchaguzi? IEBC

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ni chombo huru kinachoendesha uchaguzi. Inapaswa kuwa isiyoegemea upande — isidhibitiwe na serikali au chama chochote cha siasa.

  • Husajili wapiga kura na kusasisha daftari la wapiga kura.
  • Huweka mipaka ya maeneobunge na wadi.
  • Husajili na kuwapitisha wagombea.
  • Huendesha uchaguzi na kuhesabu kura.
  • Hutangaza matokeo na kushughulikia baadhi ya mizozo ya uchaguzi.
Art. 88

(1) Kutabuniwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka. (2) Mtu hastahili kuteuliwa kama mwachama wa Tume, ikiwa mtu huyo- (a) ashawahi kushikilia afisi au kugombea uchaguzi katika kipindi cha miaka mitano iliyotangulia kama - (i) mbunge katika ama mbunge kwenye bunge la kaunti; au (ii) mwanachama wa taasisi ya kiserikali inayosimamia chama cha kisiasa; au (b) anashikilia afisi yoyote ya taifa. (3) Mwanachama wa Tume hatashikilia afisi nyingine ya umma. (4) Tume inawajibika kuendesha na kusimamia kura za maamuzi na chaguzi katika taasisi zote zinazofanya uchaguzi au afisi zilizobuniwa na Katiba hii, na chaguzi nyingine zozote kama zilivyoagizwa na kifungu cha Sheria ya Bunge na hususan, katika- (a) usajili wa mara kwa mara wa raia kama wapiga kura; (b) usahihishaji wa mara kwa mara kwa kitabu cha usajili ya wapiga kura; (c) kuweka mipaka ya maeneobunge na wadi; (d) kudhibiti taratibu ambazo vyama hutumia kuteua wagombea uchaguzi; (e) kusuluhisha mizozo ya uchaguzi, ikiwa ni pamoja na mizozo inayohusiana na au kutokana na uteuzi lakini isiyohusisha malalamiko ya uchaguzi na mizozo inayotokana na kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi; (f) kusajili wagombea uchaguzi; (g) elimu ya mpigakura; (h) kuwezesha uchunguzi, usimamizi na tathmini ya chaguzi; (i) kudhibiti kiwango cha fedha zinazoweza kutumiwa na au kwa niaba ya mgombea au chama katika uchaguzi wowote; (j) kujenga kanuni za uchaguzi kwa wagombea na vyama vinavyogombea uchaguzi katika uchaguzi; na (k) kuchunguza utimizaji wa sheria inayotakikana chini ya Kifungu cha 82 (1) (l) kuhusiana na uteuzi wa wagombea wa vyama. (5) Tume itatumia mamlaka yake kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Katiba hii na sheria ya kitaifa iliyotungwa bungeni.

Soma kifungu kamili →

Mchakato wa uchaguzi, hatua kwa hatua

Hivi ndivyo uchaguzi unavyofanyika, kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Jiandikishe kupiga kura

Lazima uwe mwananchi wa Kenya, mwenye miaka 18 au zaidi, na ujisajili na IEBC. Jina lako huingia kwenye daftari la wapiga kura.

Art. 38

(1) Kila mwananchi ana uhuru wa kuwa na uchaguzi wa kisiasa, ikiwemo haki ya – (a) kuunda, au kushiriki katika uundaji wa chama cha kisiasa; (b) kushiriki katika shughuli za, au kusajili wanachama kwa niaba ya chama cha kisiasa; au (c) kufanyia kampeni chama cha kisiasa. (2) Kila mwananchi ana haki ya kushiriki katika uchaguzi huru, wa haki na unaofanyika mara kwa mara kwa misingi ya haki ya kupiga kura kwa wote na uhuru wa hiari ya mpiga kura kwa - (a) shirika au afisi yoyote ya umma iliyobuniwa chini ya Katiba hii na inayofanya uchaguzi; na (b) kiongozi wa afisi yoyote ya chama cha kisiasa ambacho mwananchi huyo ni mwanachama. (3) Kila raia akiwa mtu mzima ana haki pasipo na masharti yasiyo na busara,- (a) kujiandikisha kama mpiga kura; (b) kupiga kura ya siri katika uchaguzi wowote au katika kura ya maamuzi; na (c) kugombea wadhifa katika afisi ya umma, au afisi katika chama cha kisiasa ambacho yeye ni mwanachama na endapo atachaguliwa, ashike usukani.

Soma kifungu kamili →
Art. 83

(1) Mtu anastahili kusajiliwa kama mpiga kura katika chaguzi au kura za maamuzi kama mtu huyo ni raia mtu mzima; hajatangazwa kuwa na akili punguwani; na hajapatikana na hatia ya uchaguzi katika kipindi cha miaka mitano iliyotangulia. (2) raia anayestahili kusajiliwa kama mpigakura atasajiliwa kwenye kituo kimoja tu cha usajili wa kupigia kura. (3) mipango ya kiusimamizi ya usajili wa wapiga kura na uendeshaji wa chaguzi, itapangwa ili kurahisisha, na haitamnyima raia yeyote anayestahili haki ya kupiga kura au kugombea uchaguzi.

Soma kifungu kamili →

IEBC hutangaza tarehe

IEBC huweka tarehe ya uchaguzi na kuchapisha kanuni ambazo wagombea na vyama lazima wafuate.

Art. 82

(1) Bunge litatunga sheria ya kutoa nafasi ya- (a) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kuamua idadi ya maeneo-bunge kuhusu maeneo ya uchaguzi kwa wanachama wa Baraza la Kitaifa na mabaraza ya kaunti; (b) uteuzi wa wagombeaji; (c) usajili wa mara kwa mara wa raia kama wapiga kura; (d) hali ya chaguzi na kura za maamuzi. Uendeshaji na usimamizi bora wa chaguzi na kura za maamuzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa wagombeaji wa uchaguzi; na (e) usajili wa mara kwa mara wa raia wanaoishi nje ya Kenya, kama wapiga kura na kuzifahamu haki zao za kupiga kura. (2) Sheria inayotakikana na ibara ya (1) (d) itahakikisha kwamba upigaji kura katika kila uchaguzi ni- (a) rahisi; (b) wazi; na (c) inazingatia mahitaji maalumu ya- (i) watu wenye ulemavu; na (ii) watu wengine ama vikundi vya watu walio na mahitaji maalumu.

Soma kifungu kamili →

Wagombea hupitishwa

Wanaotaka kuongoza huomba kwa IEBC. Inahakikisha wanakidhi masharti, kisha wanapitishwa kugombea.

Art. 99

(1) Isipokuwa wakati mtu amepigwa marufuku katika ugombeaji chini ya Ibara ya (2), mtu anaweza kuchaguliwa kama mbunge iwapo mtu huyo- (a) amesajiliwa kama mpigakura; (b) anaafiki kiwango chochote cha kielimu, kimaadili na ana uadilifu kama inavyoagizwa kwenye Katiba hii au na Sheria ya Bunge; na (c) ameteuliwa na chama cha kisiasa au mgombeaji wa kujitegemea anayedhaminiwa - (i) na angalau wapigakura elfu moja waliosajiliwa katika eneobunge katika uchaguzi wa Baraza la Kitaifa; na (ii) na angalau wapigakura elfu mbili waliosajiliwa katika kaunti kwa uchaguzi wa Seneti. (2) Mtu hastahili kuchaguliwa kama mbunge ikiwa mtu huyo- (a) anashikilia jukumu lolote la Serikali au afisi mwingine wa umma, licha ya kuwa Mbunge; (b) amekuwa, katika kipindi cha miaka mitano inanayotangulia taratibu za uchaguzi, ameshawahi kushikilia afisi kama mwanachama wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka; (a) hakuwa raia wa Kenya kwa angalau miaka kumi inayotangulia tarehe ya uchaguzi; (b) ni mwanachama wa Baraza la Kaunti; (c) hana akili timamu; (d) mufilisi ; (e) anakabiliwa na hukumu ya kifungo cha miezi sita gerezani, kuanzia siku ya kujiandikisha kama mgombeaji, au katika tarehe ya uchaguzi; au (f) amepatikana, kwa mujibu wa sheria yoyote, kutumia vibaya afisi ya Serikali au ya umma ama kwa njia yoyote alikiuka kanuni za Sura ya Sita. (3) Mtu hazuiliwi chini ya ibara ya (2) isipokuwa tu pale ambapo uwezekano wote wa rufaa au kubadilishwa kwa kifungo kinachofaa ama pamekosekana maamuzi mengine.

Soma kifungu kamili →
Art. 137

(1) mtu anastahili kupendekezwa kuwa mgombeaji wa urais iwapo- (a) ni raia kwa kuzaliwa; (b) amehitimu kugombea uchaguzi kama mbunge; (c) ameteuliwa na chama cha kisiasa au ni mgombeaji wa kujitegemea; na (d) ameteuliwa na wapigakura wasiopungua elfu mbili kutoka kwa kila kaunti zilizo nyingi. (2) mtu hastahili kuteuliwa kuwa mgombea urais iwapo- (a) anawajibikia taifa la kigeni; (b) ni afisa wa umma, anayeshikilia afisi yoyote ya Serikali au nyingine ya umma; au (3) ibara ya (2) (b) haitatumika kwa- (a) Rais; (b) Naibu wa Rais; au (c) mbunge

Soma kifungu kamili →
Art. 193

(1) Labda azuiwe na ibara ya (2), mtu atahitimu kugombea uanachama katika baraza la kaunti kama- (a) amesajiliwa kama mpiga kura; (b) anatimiza mahitaji yote ya kielimu, tabia nzuri na maadili mema kama inavyotakikana kwa mujibu wa Katiba au Sheria ya Bunge; na (c) ama- (i) ameteuliwa na chama cha kisiasa; au (ii) ni mgombeaji wa kujitegemea aliyeungwa mkono na watu mia tano waliosajiliwa kama wapiga kura katika wadi husika. (2) Mtu hataruhusiwa kugombea kiti katika baraza la kaunti iwapo mtu huyo- (a) ana cheo Serikalini au afisi ya umma, mbali na hiyo ya baraza la kaunti anayowania kiti; (b) amekuwa na cheo katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, wakati wowote ule katika miaka mitano iliyotangulia tarehe ya uchaguzi. (c) hajakuwa raia wa Kenya kwa miaka isiyopungua kumi iliyotangulia tarehe ya uchaguzi; (d) hana akili timamu; (e) ni mufilisi; (f) anatumikia kifungo gerezani cha miezi sita au zaidi; au (g) amepatikana, kulingana na sheria yoyote, kwamba ametumia vibaya afisi ya umma ama kwa njia yoyote ile kukiuka kanuni za Sura ya sita. (3) Mtu hatazuiwa kulingana na ibara ya (2) ila tu kama uwezekano wa kukata rufaa ama kesi yake kushughulikiwa upya kwa kifungo chake na mbinu zote za kujitetea zimekwisha.

Soma kifungu kamili →

Kipindi cha kampeni

Wagombea hueleza mipango yao na kuomba kura. Kuna kanuni za matumizi, utangazaji wa haki na kuepuka vurugu.

Art. 81

Mfumo wa uchaguzi utazingatia kanuni zifuatazo- (a) uhuru wa raia wa kutekeleza haki zao za kisiasa chini ya Ibara ya 38; (b) sio zaidi ya thuluthi mbili ya wanachama wa mashirika ya umma yatakayoshiriki uchaguzi wa wanachama watakuwa ya jinsia sawa; (c) uwakilishi wenye usawa wa watu walio na ulemavu; (d) haki ya kupiga kura kwa wote katika misingi ya haki ya uwakilishwaji na usawa wa kura; na (e) chaguzi za haki na usawa, ambazo ni - (i) za kura ya siri; (ii) huru na zisizo na ghasia, vitisho, ushawishi usiofaa, au ufisadi; (iii) zinazoendeshwa na halmashauri huru; (iv) wazi; na (v) zinazofanywa kwa njia zisizopendelea upande wowote, katikati, bora, kamilifu na zilizo na uwajibikaji.

Soma kifungu kamili →
Art. 82

(1) Bunge litatunga sheria ya kutoa nafasi ya- (a) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kuamua idadi ya maeneo-bunge kuhusu maeneo ya uchaguzi kwa wanachama wa Baraza la Kitaifa na mabaraza ya kaunti; (b) uteuzi wa wagombeaji; (c) usajili wa mara kwa mara wa raia kama wapiga kura; (d) hali ya chaguzi na kura za maamuzi. Uendeshaji na usimamizi bora wa chaguzi na kura za maamuzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa wagombeaji wa uchaguzi; na (e) usajili wa mara kwa mara wa raia wanaoishi nje ya Kenya, kama wapiga kura na kuzifahamu haki zao za kupiga kura. (2) Sheria inayotakikana na ibara ya (1) (d) itahakikisha kwamba upigaji kura katika kila uchaguzi ni- (a) rahisi; (b) wazi; na (c) inazingatia mahitaji maalumu ya- (i) watu wenye ulemavu; na (ii) watu wengine ama vikundi vya watu walio na mahitaji maalumu.

Soma kifungu kamili →

Siku ya kupiga kura

Wapiga kura huenda kituo chao cha kupiga kura na kupiga kura kwa faragha. Mtu mmoja, kura moja.

Art. 38

(1) Kila mwananchi ana uhuru wa kuwa na uchaguzi wa kisiasa, ikiwemo haki ya – (a) kuunda, au kushiriki katika uundaji wa chama cha kisiasa; (b) kushiriki katika shughuli za, au kusajili wanachama kwa niaba ya chama cha kisiasa; au (c) kufanyia kampeni chama cha kisiasa. (2) Kila mwananchi ana haki ya kushiriki katika uchaguzi huru, wa haki na unaofanyika mara kwa mara kwa misingi ya haki ya kupiga kura kwa wote na uhuru wa hiari ya mpiga kura kwa - (a) shirika au afisi yoyote ya umma iliyobuniwa chini ya Katiba hii na inayofanya uchaguzi; na (b) kiongozi wa afisi yoyote ya chama cha kisiasa ambacho mwananchi huyo ni mwanachama. (3) Kila raia akiwa mtu mzima ana haki pasipo na masharti yasiyo na busara,- (a) kujiandikisha kama mpiga kura; (b) kupiga kura ya siri katika uchaguzi wowote au katika kura ya maamuzi; na (c) kugombea wadhifa katika afisi ya umma, au afisi katika chama cha kisiasa ambacho yeye ni mwanachama na endapo atachaguliwa, ashike usukani.

Soma kifungu kamili →
Art. 86

Katika kila uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itahakikisha kwamba- (a) katika njia yoyote ya upigaji kura itakayotumiwa, mfumo unakuwa rahisi, sahihi, wa kuthibitika, salama, unaowajibika na ulio na uwazi; (b) kura zinazopigwa zinahesabiwa, kuorodheshwa na matokeo kutangazwa moja kwa moja na afisa msimamizi wa kituo cha upigaji kura hapo kituoni; (c) matokeo kutoka kwa vituo vingine vya upigaji kura yanajumlishwa kwa uwazi na kutangazwa moja kwa moja na afisa msimamizi wa kituo cha upigaji kura; na miundo na taratibu mwafaka zimewekwa ili kuondoa uwezekano wa kuhusishwa kwa mienendo yoyote mibaya, ukiwemo uhifadhi salama wa vifaa vya uchaguzi.

Soma kifungu kamili →

Kuhesabu na kujumlisha

Kura huhesabiwa kwenye kila kituo cha kupiga kura na kutangazwa hapo. Kisha matokeo hujumlishwa kwa uwazi katika ngazi ya eneobunge.

Art. 86

Katika kila uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itahakikisha kwamba- (a) katika njia yoyote ya upigaji kura itakayotumiwa, mfumo unakuwa rahisi, sahihi, wa kuthibitika, salama, unaowajibika na ulio na uwazi; (b) kura zinazopigwa zinahesabiwa, kuorodheshwa na matokeo kutangazwa moja kwa moja na afisa msimamizi wa kituo cha upigaji kura hapo kituoni; (c) matokeo kutoka kwa vituo vingine vya upigaji kura yanajumlishwa kwa uwazi na kutangazwa moja kwa moja na afisa msimamizi wa kituo cha upigaji kura; na miundo na taratibu mwafaka zimewekwa ili kuondoa uwezekano wa kuhusishwa kwa mienendo yoyote mibaya, ukiwemo uhifadhi salama wa vifaa vya uchaguzi.

Soma kifungu kamili →

Matokeo hutangazwa

IEBC hutangaza washindi. Kwa Rais, mshindi lazima apate zaidi ya nusu ya kura zote na angalau 25% katika kaunti 24.

Art. 138

(1) iwapo ni mgombea urais mmoja tu atateuliwa, mgombeaji huyo atatangazwa kuwa ameteuliwa. (2) iwapo wagombeaji wa urais wawili au zaidi watateuliwa, uchaguzi wa urais utafanyika katika kila eneobunge. (3) Katika uchaguzi wa urais- (a) wapigakura wote waliosajiliwa kama wapigakura kwa kusudi la uchaguzi wa wabunge wana haki ya kupiga kura. (b) uchaguzi utakuwa kwa njia ya siri katika siku ambayo imeelezewa kwenye ibara ya 101(1) na kwa wakati, mahali na kwa njia ambayo imeamriwa chini ya Sheria ya Bunge; na (c) baada ya kuhesabiwa kwa kura katika vituo vya kupigia kura, Tume Huru ya Uchaguzi na mipaka itahesabu na kuhakikisha hesabu ya kura na kutangaza matokeo. (4) Mgombea urais atatangazwa kuwa Rais iwapo atapokea- (a) zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa katika uchaguzi; na (b) angalau asilimia ishirini na tano ya kura zilizopigwa katika kila kaunti na kaunti ziwe zaidi ya nusu ya kaunti zote kwa jumla. (5) Iwapo hakuna mgombeaji amechaguliwa, uchaguzi mwingine utafanyika upya katika kipindi cha siku thelathini baada ya uchaguzi uliopita, na katika uchaguzi huo mpya, wagombeji watakuwa- (a) mgombeaji au wagombeaji ambao walipata kura nyingi zaidi; na (b) mgombeaji au wagombeaji ambao walipata idadi ya pili ya wingi wa kura. (6) pale ambapo wagombeaji zaidi ya mmoja wamepata idadi kubwa zaidi ya kura, ibara ya (5) (b) haitatumika na wagombeaji pekee katika uchaguzi mpya watakuwa wale ambao wameelezewa katika Ibara ya (5) (a). (7) mgombeaji ambaye atapata idadi kubwa zaidi ya kura kwenye uchaguzi mpya, atatangazwa kuwa Rais. (8) uchaguzi wa urais utafutiliwa mbali na uchaguzi mwingine mpya kufanyika iwapo- (a) hakuna mtu ambaye ameteuliwa kama mgombea uchaguzi kabla ya kumalizika kwa kipindi kilichowekwa cha kuwasilisha watakaoteuliwa; (b) mgombea uchaguzi wa urais au naibu wa Rais ataaga dunia mnamo au kabla ya tarehe iliyopangiwa kufanyika uchaguzi; au (c) mgombea uchaguzi ambaye alistahili kutangazwa kuwa Rais, kuaga dunia kabla ya kutangazwa kama Rais. (9) uchaguzi mpya wa urais chini ya ibara ya (8) utafanyika katika muda wa siku sitini baada ya tarehe iliyokuwa imewekwa ya uchaguzi uliotangulia. (10) Katika muda wa siku saba baada uchaguzi wa urais, mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka- (a) atangaza matokeo ya uchaguzi; na (b) atawasilisha ripoti iliyoandikwa ya matokeo ya uchaguzi kwa Jaji Mkuu na Rais aliye mamlakani.

Soma kifungu kamili →

Mizozo huenda mahakamani

Kama mtu anaamini matokeo si sahihi, anaweza kuyapinga mahakamani. Mahakama Kuu husikiliza maombi kuhusu uchaguzi wa Rais.

Art. 87

(1) Bunge litatunga sheria ya kubuniwa kwa mifumo ya kusuluhishwa kwa haraka mizozo ya uchaguzi. (2) Malalamiko kuhusu uchaguzi, isipokuwa uchaguzi wa urais, yatawasilishwa katika kipindi cha siku ishirini na nane baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka. (3) Kukabidhiwa kwa mashtaka hayo kunaweza kuwa kwa moja kwa moja au kupitia kwa tangazo katika gazeti linalosambazwa kote nchini.

Soma kifungu kamili →
Art. 140

(1) Mtu anaweza kuwasilisha malalamiko katika Mahakama ya Juu kupinga uchaguzi wa Rais mteule katika muda wa siku saba baada ya tarehe ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais. (2) katika muda wa siku kumi na nne baada ya kuwasilishwa kwa malalamiko, Mahakaya ya Juu itasikiza na kuamua kesi hiyo na uamuzi wake utakuwa wa mwisho. (3) Iwapo Mahakama ya Juu itaamua kuwa uchaguzi wa Rais Mteule si halali, uchaguzi mpya utafanyika katika muda wa siku sitini baada ya uamuzi huo.

Soma kifungu kamili →

Nini hufanya uchaguzi uwe huru na wa haki

Katiba huweka kanuni ili matokeo yaakisi chaguo la wananchi kwa kweli.

IEBC huru

Chombo kinachoendesha uchaguzi lazima kiwe kisichoegemea upande na kisimpendelee mtu.

Art. 81

Mfumo wa uchaguzi utazingatia kanuni zifuatazo- (a) uhuru wa raia wa kutekeleza haki zao za kisiasa chini ya Ibara ya 38; (b) sio zaidi ya thuluthi mbili ya wanachama wa mashirika ya umma yatakayoshiriki uchaguzi wa wanachama watakuwa ya jinsia sawa; (c) uwakilishi wenye usawa wa watu walio na ulemavu; (d) haki ya kupiga kura kwa wote katika misingi ya haki ya uwakilishwaji na usawa wa kura; na (e) chaguzi za haki na usawa, ambazo ni - (i) za kura ya siri; (ii) huru na zisizo na ghasia, vitisho, ushawishi usiofaa, au ufisadi; (iii) zinazoendeshwa na halmashauri huru; (iv) wazi; na (v) zinazofanywa kwa njia zisizopendelea upande wowote, katikati, bora, kamilifu na zilizo na uwajibikaji.

Soma kifungu kamili →
Art. 88

(1) Kutabuniwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka. (2) Mtu hastahili kuteuliwa kama mwachama wa Tume, ikiwa mtu huyo- (a) ashawahi kushikilia afisi au kugombea uchaguzi katika kipindi cha miaka mitano iliyotangulia kama - (i) mbunge katika ama mbunge kwenye bunge la kaunti; au (ii) mwanachama wa taasisi ya kiserikali inayosimamia chama cha kisiasa; au (b) anashikilia afisi yoyote ya taifa. (3) Mwanachama wa Tume hatashikilia afisi nyingine ya umma. (4) Tume inawajibika kuendesha na kusimamia kura za maamuzi na chaguzi katika taasisi zote zinazofanya uchaguzi au afisi zilizobuniwa na Katiba hii, na chaguzi nyingine zozote kama zilivyoagizwa na kifungu cha Sheria ya Bunge na hususan, katika- (a) usajili wa mara kwa mara wa raia kama wapiga kura; (b) usahihishaji wa mara kwa mara kwa kitabu cha usajili ya wapiga kura; (c) kuweka mipaka ya maeneobunge na wadi; (d) kudhibiti taratibu ambazo vyama hutumia kuteua wagombea uchaguzi; (e) kusuluhisha mizozo ya uchaguzi, ikiwa ni pamoja na mizozo inayohusiana na au kutokana na uteuzi lakini isiyohusisha malalamiko ya uchaguzi na mizozo inayotokana na kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi; (f) kusajili wagombea uchaguzi; (g) elimu ya mpigakura; (h) kuwezesha uchunguzi, usimamizi na tathmini ya chaguzi; (i) kudhibiti kiwango cha fedha zinazoweza kutumiwa na au kwa niaba ya mgombea au chama katika uchaguzi wowote; (j) kujenga kanuni za uchaguzi kwa wagombea na vyama vinavyogombea uchaguzi katika uchaguzi; na (k) kuchunguza utimizaji wa sheria inayotakikana chini ya Kifungu cha 82 (1) (l) kuhusiana na uteuzi wa wagombea wa vyama. (5) Tume itatumia mamlaka yake kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Katiba hii na sheria ya kitaifa iliyotungwa bungeni.

Soma kifungu kamili →

Kura ya faragha

Hakuna anayepaswa kuona au kulazimisha kura yako.

Art. 38

(1) Kila mwananchi ana uhuru wa kuwa na uchaguzi wa kisiasa, ikiwemo haki ya – (a) kuunda, au kushiriki katika uundaji wa chama cha kisiasa; (b) kushiriki katika shughuli za, au kusajili wanachama kwa niaba ya chama cha kisiasa; au (c) kufanyia kampeni chama cha kisiasa. (2) Kila mwananchi ana haki ya kushiriki katika uchaguzi huru, wa haki na unaofanyika mara kwa mara kwa misingi ya haki ya kupiga kura kwa wote na uhuru wa hiari ya mpiga kura kwa - (a) shirika au afisi yoyote ya umma iliyobuniwa chini ya Katiba hii na inayofanya uchaguzi; na (b) kiongozi wa afisi yoyote ya chama cha kisiasa ambacho mwananchi huyo ni mwanachama. (3) Kila raia akiwa mtu mzima ana haki pasipo na masharti yasiyo na busara,- (a) kujiandikisha kama mpiga kura; (b) kupiga kura ya siri katika uchaguzi wowote au katika kura ya maamuzi; na (c) kugombea wadhifa katika afisi ya umma, au afisi katika chama cha kisiasa ambacho yeye ni mwanachama na endapo atachaguliwa, ashike usukani.

Soma kifungu kamili →
Art. 86

Katika kila uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itahakikisha kwamba- (a) katika njia yoyote ya upigaji kura itakayotumiwa, mfumo unakuwa rahisi, sahihi, wa kuthibitika, salama, unaowajibika na ulio na uwazi; (b) kura zinazopigwa zinahesabiwa, kuorodheshwa na matokeo kutangazwa moja kwa moja na afisa msimamizi wa kituo cha upigaji kura hapo kituoni; (c) matokeo kutoka kwa vituo vingine vya upigaji kura yanajumlishwa kwa uwazi na kutangazwa moja kwa moja na afisa msimamizi wa kituo cha upigaji kura; na miundo na taratibu mwafaka zimewekwa ili kuondoa uwezekano wa kuhusishwa kwa mienendo yoyote mibaya, ukiwemo uhifadhi salama wa vifaa vya uchaguzi.

Soma kifungu kamili →

Kanuni za haki za kampeni

Vyama na wagombea lazima watendewe kwa usawa na wafuate kanuni.

Art. 81

Mfumo wa uchaguzi utazingatia kanuni zifuatazo- (a) uhuru wa raia wa kutekeleza haki zao za kisiasa chini ya Ibara ya 38; (b) sio zaidi ya thuluthi mbili ya wanachama wa mashirika ya umma yatakayoshiriki uchaguzi wa wanachama watakuwa ya jinsia sawa; (c) uwakilishi wenye usawa wa watu walio na ulemavu; (d) haki ya kupiga kura kwa wote katika misingi ya haki ya uwakilishwaji na usawa wa kura; na (e) chaguzi za haki na usawa, ambazo ni - (i) za kura ya siri; (ii) huru na zisizo na ghasia, vitisho, ushawishi usiofaa, au ufisadi; (iii) zinazoendeshwa na halmashauri huru; (iv) wazi; na (v) zinazofanywa kwa njia zisizopendelea upande wowote, katikati, bora, kamilifu na zilizo na uwajibikaji.

Soma kifungu kamili →

Hakuna vurugu au udanganyifu

Sheria inakataza rushwa, vitisho na vurugu wakati wa uchaguzi.

Art. 81

Mfumo wa uchaguzi utazingatia kanuni zifuatazo- (a) uhuru wa raia wa kutekeleza haki zao za kisiasa chini ya Ibara ya 38; (b) sio zaidi ya thuluthi mbili ya wanachama wa mashirika ya umma yatakayoshiriki uchaguzi wa wanachama watakuwa ya jinsia sawa; (c) uwakilishi wenye usawa wa watu walio na ulemavu; (d) haki ya kupiga kura kwa wote katika misingi ya haki ya uwakilishwaji na usawa wa kura; na (e) chaguzi za haki na usawa, ambazo ni - (i) za kura ya siri; (ii) huru na zisizo na ghasia, vitisho, ushawishi usiofaa, au ufisadi; (iii) zinazoendeshwa na halmashauri huru; (iv) wazi; na (v) zinazofanywa kwa njia zisizopendelea upande wowote, katikati, bora, kamilifu na zilizo na uwajibikaji.

Soma kifungu kamili →
Art. 82

(1) Bunge litatunga sheria ya kutoa nafasi ya- (a) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kuamua idadi ya maeneo-bunge kuhusu maeneo ya uchaguzi kwa wanachama wa Baraza la Kitaifa na mabaraza ya kaunti; (b) uteuzi wa wagombeaji; (c) usajili wa mara kwa mara wa raia kama wapiga kura; (d) hali ya chaguzi na kura za maamuzi. Uendeshaji na usimamizi bora wa chaguzi na kura za maamuzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa wagombeaji wa uchaguzi; na (e) usajili wa mara kwa mara wa raia wanaoishi nje ya Kenya, kama wapiga kura na kuzifahamu haki zao za kupiga kura. (2) Sheria inayotakikana na ibara ya (1) (d) itahakikisha kwamba upigaji kura katika kila uchaguzi ni- (a) rahisi; (b) wazi; na (c) inazingatia mahitaji maalumu ya- (i) watu wenye ulemavu; na (ii) watu wengine ama vikundi vya watu walio na mahitaji maalumu.

Soma kifungu kamili →

Baada ya matokeo

Nini hufanyika washindi wanapojulikana.

Mshindi huapishwa

Viongozi wa umma huapa kabla ya kuchukua ofisi.

Art. 141

(1) kuapishwa kwa Rais Mteule kutafanyika wazi na mbele ya Jaji Mkuu na ikiwa Jaji Mkuu hayupo, basi mbele ya Naibu jaji mkuu. (2) Rais Mteule ataapishwa Jumanne ya kwanza itakayofuata- (a) siku kumi na nne baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Urais isipokuwa matangazo hayo yawe yamepingwa kulingana na Kifungu cha 140; ama (b) siku ya saba kufuatia tarehe ambayo mahakama inatoa uamuzi na kutangaza kuwa uchaguzi ulikuwa halali, ikiwa malalamiko yoyote yalikuwa yamewasilishwa chini ya Kifungu cha 140. (3) Rais Mteule anachukua hatamu za Urais kwa kuchukua na kutia sahihi kiapo cha uaminifu; na kiapo cha kutekeleza majukumu ya Urais kama ilivyoamriwa katika Ratiba ya Tatu. (4) Bunge kupitia kwa sheria itatoa taratibu za sherehe za kuapishwa kwa Rais-mteule.

Soma kifungu kamili →
Art. 148

(1) Kila mgombea uchaguzi wa Urais atateua mtu ambaye amehitimu kuchaguliwa kama Rais, kama mgombeaji wa Naibu wa Rais. (2) Kwa sababu ya ibara ya (1), hakutakuwa na utaratibu tofauti wa uteuzi wa Naibu wa Rais na kifungu cha 137 (1) (d) hakitatumika kwa mgombeaji kiti cha Naibu wa Rais. (3) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itatangaza yule ambaye ameteuliwa na Rais mteule kuwa ndiye Naibu wa Rais. (4) Kuapishwa kwa Naibu wa Rais mteule kutafanyika mbele ya Jaji Mkuu au iwapo Jaji Mkuu hayupo, mbele ya Naibu wa Jaji Mkuu na wananchi. (5) Naibu wa rais mteule atachukua hatamu za afisi kwa- (a) Kula kiapo cha uaminifu; na (b) Kiapo cha kutekeleza majukumu ya afisi kama ilivyoidhinishwa katika Ratiba ya Tatu. Kipindi cha afisi ya Naibu wa rais kitaanza kutumika kutoka siku ya kuapishwa kwa Naibu wa rais na kukoma- Wakati mtu atakayechaguliwa kama Rais anayefuata katika uchaguzi chini ya Kifungu cha (136) (2) (a) ataapishwa; Wakati Naibu wa rais atachukua mamlaka ya Rais; au Katika kijiuzulu , kifo au kuachishwa kazi kwa Naibu wa rais. Naibu wa rais anaweza, kwa wakati wowote, kujiuzulu kwa kumwandikiia barua Rais na kujiuzulu huku kutaanza kutekelezwa saa na tarehe iliyobainishwa katika barua hiyo au iwapo tarehe haijabainishwa, adhuhuri ya siku ya kupokelewa kwa barua hiyo. Hakuna mtu yoyote atakayehudumu kwa zaidi ya vipindi viwili kama Naibu wa rais.

Soma kifungu kamili →

Walioshindwa wanaweza kupinga

Maombi ya uchaguzi humwomba mahakama ichunguze kama matokeo yalikuwa halali.

Art. 87

(1) Bunge litatunga sheria ya kubuniwa kwa mifumo ya kusuluhishwa kwa haraka mizozo ya uchaguzi. (2) Malalamiko kuhusu uchaguzi, isipokuwa uchaguzi wa urais, yatawasilishwa katika kipindi cha siku ishirini na nane baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka. (3) Kukabidhiwa kwa mashtaka hayo kunaweza kuwa kwa moja kwa moja au kupitia kwa tangazo katika gazeti linalosambazwa kote nchini.

Soma kifungu kamili →
Art. 140

(1) Mtu anaweza kuwasilisha malalamiko katika Mahakama ya Juu kupinga uchaguzi wa Rais mteule katika muda wa siku saba baada ya tarehe ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais. (2) katika muda wa siku kumi na nne baada ya kuwasilishwa kwa malalamiko, Mahakaya ya Juu itasikiza na kuamua kesi hiyo na uamuzi wake utakuwa wa mwisho. (3) Iwapo Mahakama ya Juu itaamua kuwa uchaguzi wa Rais Mteule si halali, uchaguzi mpya utafanyika katika muda wa siku sitini baada ya uamuzi huo.

Soma kifungu kamili →

Uchaguzi mdogo

Kama nafasi inabaki wazi kati ya uchaguzi mkuu, uchaguzi mdogo huijaza.

Art. 101

(1) Uchaguzi mkuu wa wabunge utafanyika Jumanne ya pili ya mwezi wa Agosti katika kila mwaka wa tano. (2) panapotokea nafasi katika afisi ya mbunge wa Baraza la Kitaifa, lililotajwa chini ya Kifungu cha 97 (1) (c), au katika Seneti chini ya Kifungu cha 98 (1) (b), (c) ama (d), Spika mhusika, katika kipindi cha siku ishirini na moja za kutokea nafasi hiyo ya kazi, atatoa notisi kwa maandishi kuhusu nafasi hiyo ya kazi kwa- (a) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka; na (b) chama cha kisiasa ambacho kupitia kwa orodha yake ya chama ndipo mwanachama huyo alipokuwa amechaguliwa au kuteuliwa. (3) Nafasi hiyo iliyotajwa katika Ibara ya (2) kwa, kuambatana na Ibara ya (5), itajazwa kwa namna iliyoagizwa na Sheria ya Bunge ndani ya muda wa siku ishirini na moja baada ya kutangazwa na Spika mhusika. (4) Panapotokea nafasi ya kazi katika afisi ya mwanachama wa Baraza la Kitaifa aliyechaguliwa chini ya Kifungu cha 97 (1) (a) au (b), au wa Seneti aliyechaguliwa chini ya Kifungu cha 98 (1) (a)- (a) Spika mhusika, kwa muda wa siku ishirini na moja baada ya kutokea kwa nafasi hii, atatoa notisi kuhusu nafasi hii kwa kuiandikia Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka; na (b) uchaguzi mdogo utafanyika katika muda wa siku tisini baada ya kutokea kwa nafasi hiyo ya kazi, kuambatana na ibara ya (5). (5) Nafasi iliyotajwa katika ibara ya (4) haitajazwa katika kipindi cha miezi mitatu inayotangulia uchaguzi mkuu.

Soma kifungu kamili →

Nani anafanya nini katika uchaguzi

Wapiga kuraHujiandikisha na kuchagua viongozi kwa faragha.
IEBCHusajili wapiga kura, hupitisha wagombea, huendesha na kuhesabu uchaguzi.
Wagombea na vyamaHufanya kampeni na kufuata kanuni za uchaguzi.
MahakamaHuamua mizozo na maombi ya uchaguzi.
WananchiWana mamlaka; uchaguzi ni jinsi wanavyoyapa na kuyarudisha.

Soma vifungu halisi

Kila hoja kwenye ukurasa huu inatoka katika Katiba. Gusa rejeo kuona kifungu halisi.

    Tafuta →