Wananchi ndio wakubwa
Kenya ni ya watu wote. Viongozi huongoza tu kwa sababu wananchi wanawachagua.
Art. 1(1)
(1) Mamlaka yote makuu ni ya wananchi wa Kenya na yanaweza kutekelezwa tu kulingana na Katiba hii.
Soma kifungu kamili →Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho
Serikali
Fikiria Kenya ni timu kubwa. Tuje tuone nani anafanya nini, kuanzia juu hadi chini.
Kenya ni ya watu wote. Viongozi huongoza tu kwa sababu wananchi wanawachagua.
(1) Mamlaka yote makuu ni ya wananchi wa Kenya na yanaweza kutekelezwa tu kulingana na Katiba hii.
Soma kifungu kamili →Ni sheria muhimu kuliko zote. Hata Rais lazima aifuate.
(1) Katiba hii ni sheria kuu ya Jamhuri na inaunganisha asasi zote za nchi katika viwango vyote viwili vya Serikali na watu wote.
Soma kifungu kamili →Baadhi ya maamuzi ni ya nchi nzima. Mengine ni ya eneo lako tu.
Inashughulikia mambo makubwa ya nchi nzima, kama jeshi na barabara kubwa.
(1) Eneo la Kenya limegawanywa katika kaunti zilizotajwa katika Mpangilio wa Kwanza.
Soma kifungu kamili →Inashughulikia mambo karibu nawe, kama zahanati, masoko na barabara ndogo.
(2) Serikali katika viwango vya kitaifa na kaunti ni tofauti na zinategemeana na Zitaendesha mahusiano yao ya uelewanaji kwa misingi ya mashauriano na ushirikiano.
Soma kifungu kamili →Timu tatu hufanya kazi pamoja. Hakuna anayefanya kila kitu peke yake.
Bunge
(1) Mamlaka ya utungaji wa sheria ya Jamhuri hii inatokana na wananchi na katika kiwango cha kitaifa, yamekabidhiwa kwa na kutekelezwa na Bunge. (2) Bunge hufuatilia uanuwai wa taifa, huwakilisha nia ya wananchi, na hutekeleza Mamlaka yao. (3) Bunge linaweza kukubali na kupitisha marekebisho kwenye Katiba hii na kubadilisha mipaka ya kaunti kama inavyoagizwa katika Katiba hii; (4) Bunge litalinda Katiba hii na kudumisha utawala wa kidemokrasia katika Jamhuri hii. (5) Hakuna mtu yeyote au asasi yoyote, isipokuwa Bunge, itakayokuwa na mamlaka ya kuunda masharti yatakayokuwa na nguvu za kisheria nchini Kenya isipokuwa kwa amri ya Katiba hii iliyokabidhiwa Bunge au kwa Sheria ya Bunge. (6) Sheria ya Bunge, au sheria ya kaunti, inayoipatia asasi yoyote ya Serikali, afisa wa Serikali, au mtu yeyote mamlaka ya kutunga masharti au sheria na kuipatia nguvu za kisheria nchini Kenya, kama inavyokusudiwa katika Ibara ya (5), itaeleza bayana na kwa hakika shabaha na malengo ya kukabidhiwa mamlaka haya, viwango vya mamlaka, hali na upeo wa sheria zitakavyotungwa, na kanuni na viwango vya ubora vinavyotumika kisheria na vilivyobuniwa chini ya mamlaka haya.
Soma kifungu kamili →(1) Baraza la Kitaifa linawakilisha watu wa maeneobunge na walio na maslahi maalumu katika Baraza la Kitaifa. (2) Baraza la Kitaifa hushauriana kuhusu na kusuluhisha masuala yenye umuhimu mkubwa kwa watu. (3) Baraza la Kitaifa linatunga sheria kwa kuzingatia Sehemu ya 4 ya Sura hii. (4) Baraza la Kitaifa - (a) hubainisha ugavi wa mapato ya kitaifa kati ya ngazi za Serikali, kama inavyoagizwa katika Sehemu ya 4 ya Sura ya Kumi na Mbili; (b) hugawa hazina ya fedha kwa matumizi ya Serikali ya kitaifa na asasi nyingine za Serikali ya kitaifa; na (c) hutekeleza usimamizi wa jumla wa mapato ya kitaifa pamoja na matumizi yake. (5) Baraza la Kitaifa- (a) linachunguza utendakazi wa Rais afisini, Naibu wa rais na maafisa wengine wa Serikali na ikiwezekana kuchukua hatua za kuwatoa afisini; na (b) litasimamia asasi za Serikali; (6) Baraza la Kitaifa litaidhinisha tangazo la vita na kutathmini ongezeko la hali ya hatari nchini.
Soma kifungu kamili →Rais na serikali
(1) Mamlaka kuu ya Serikali yanatokana na Wakenya na yatatekelezwa kwa mujibu wa Katiba hii.
Soma kifungu kamili →(1) Rais - (a) ndiye Kiongozi wa Taifa na Serikali; (b) anatekeleza mamlaka makuu ya Jamhuri kwa usaidizi wa Naibu wa Rais na Mawaziri; (c) ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Kenya; (d) ndiye mwenyekiti wa Baraza la Kitaifa la Usalama (e) ni ishara ya umoja wa kitaifa. (2) Rais - (a) ataiheshimu, kuifuata na kuilinda Katiba; (b) ataulinda uhuru wa Jamhuri ya Kenya. (c) atakuza na kudumisha umoja wa taifa. (d) atakuza heshima ya uanuwai wa watu wa Kenya; na (e) kuhakikisha ulinzi wa uhuru na haki za kimsingi za raia na utawala wa sheria. (3) Rais hatasimamia afisi nyingine yoyote ya Serikali au ya umma.
Soma kifungu kamili →Mahakama
(1) Mamlaka ya Mahakama yanatokana na watu, yanajikita katika mahakama na mahakama maalum zinazobuniwa kulingana na Katiba hii. (2) Katika kutekeleza majukumu ya kimahakama, mahakama na mahakama maalum zitaongozwa na kanuni zifuatazo- (a) haki itatendwa kwa kila mtu bila kuzingatia hadhi ; (b) Haki haitacheleweshwa; (c) njia m’badala za kusuluhisha kesi zikiwemo msamaha, mashauriano, na maridhiano na njia za kitamaduni za kusuluhisha migogoro zitaimarishwa, kwa mujibu wa ibara ya (3); (d) haki itatolewa kwa kuzingatia matatizo yaliyopo ya utaratibu wa kitaalamu; na (e) lengo na kanuni za Katiba hii zitatunzwa na kuendelezwa. (3) Mbinu za kitamaduni za utatuaji wa migogoro hazitatumiwa kwa njia ambayo- (a) itakiuka Sheria za Haki; (b) itagongana na haki na maadili au kusababisha matokeo yatakayogongana na haki na maadili; (c) haiambatani na Katiba hii au sheria yoyote iliyoandikwa.
Soma kifungu kamili →(1) Katika utekelezaji wa mamlaka ya mahakama, Mahakama kama ilivyoundwa chini ya kifungu cha 161, itazingatia Katiba hii pamoja na sheria na haitadhibitiwa wala kuelekezwa na mtu yeyote mwingine au halmashauri. (2) Afisi ya jaji wa mahakama ya Mamlaka Kuu haitafutiliwa mbali wakati ambapo kuna afisa anayeshikilia wadhifa huo. (3) Mishahara na marupurupu yanayofaa kulipwa, au kuhusiana na, majaji yatatoka kwa Mfuko wa Jumla wa Serikali. (4) Kulingana na Kifungu cha 168 (6), mishahara na marupurupu inayofaa kulipwa, au kuhusiana na majaji haitabadilishwa kwa njia itakayowaathiri, na marupurupu ya kustaafu ya jaji hayatabadilishwa ili kumuathiri jaji mstaafu katika maisha yake ya uhai. (5) Mwanachama wa mahakama hatawajibika katika hatua au kesi kuhusiana na chochote watakachofanya au watakachokosa kufanya kwa nia njema katika utendaji kazi wa kisheria kwa kutekeleza majukumu ya mahakama.
Soma kifungu kamili →Kaunti yako ina wasaidizi wake, karibu na nyumbani.
Malengo ya Serikali ya ugatuzi ni- (a) kuhakikisha kuwa kuna mamlaka ya kidemokrasia na uwajibikiaji wa Serikali ; (b) kuhimiza umoja wa kitaifa kwa kutambua uanuwai wa jamii mbalimbali; (c) kuwapa watu katika kila ngazi mamlaka ya kujitawala na kushiriki katika matumizi ya mamlaka ya Serikali katika kufanya maamuzi ya mambo yanyowaathiri; (d) kutambua haki za jamii zote katika kusimamia masuala ya jamii zao na kujiendeleza zaidi; (e) kulinda na kuhamasisha maslahi na haki za jamii za watu walio wachache na zile za watu waliotengwa; (f) kustawisha miradi ya kijamii na kiuchumi na utoaji wa huduma za karibu na zilizo rahisi ili kumfikia kila mtu nchini Kenya; (g) kuhakikisha kuna ugavi sawa wa rasilmali zote za kijamii na za kitaifa kote nchini. (h) kufanikisha ugatuzi wa mamlaka ya taasisi za Serikali, uendeshaji wake wa shughuli ama huduma kutoka mji mkuu wa Kenya; na (i) kuhakikisha kuna kudhibiti na kugawana mamlaka kwa njia iliyo sawa.
Soma kifungu kamili →Kama mchezo wenye waamuzi, kila timu inaweza kuzuia nyingine kufanya kosa.
Kama mtu anavunja kitabu cha sheria, mahakama zinaweza kusema acha.
(1) Mamlaka ya Mahakama yanatokana na watu, yanajikita katika mahakama na mahakama maalum zinazobuniwa kulingana na Katiba hii. (2) Katika kutekeleza majukumu ya kimahakama, mahakama na mahakama maalum zitaongozwa na kanuni zifuatazo- (a) haki itatendwa kwa kila mtu bila kuzingatia hadhi ; (b) Haki haitacheleweshwa; (c) njia m’badala za kusuluhisha kesi zikiwemo msamaha, mashauriano, na maridhiano na njia za kitamaduni za kusuluhisha migogoro zitaimarishwa, kwa mujibu wa ibara ya (3); (d) haki itatolewa kwa kuzingatia matatizo yaliyopo ya utaratibu wa kitaalamu; na (e) lengo na kanuni za Katiba hii zitatunzwa na kuendelezwa. (3) Mbinu za kitamaduni za utatuaji wa migogoro hazitatumiwa kwa njia ambayo- (a) itakiuka Sheria za Haki; (b) itagongana na haki na maadili au kusababisha matokeo yatakayogongana na haki na maadili; (c) haiambatani na Katiba hii au sheria yoyote iliyoandikwa.
Soma kifungu kamili →Rais anaweza kuomba Bunge lifikirie tena kuhusu sheria.
(1) Katika kipindi cha muda wa siku kumi na nne baada ya kupokea Mswada, Rais- (a) ataweka saini; au (b) ataurejesha Mswada Bungeni ili kuchunguzwa upya na Bunge huku likitilia maanani sababu alizo nazo Rais za kutouidhinisha mswada huo. (2) Iwapo Rais ataurejesha Mswada bungeni kuchunguzwa upya, Bunge kwa kuzingatia taratibu zinazofaa kama zilivyotajwa katika sehemu hii, linaweza- (a) kuurekebisha Mswada huo kwa kuangazia sababu muhimu alizotoa Rais; au (b) kuupitisha Mswada huo kwa mara ya pili bila kufanya marekebisho. (3) Iwapo Bunge limerekebisha Mswada huo huku likitilia maanani kikamilifu hoja za Rais, Spika anayehusika atampelekea Rais tena ili aweke sahihi. (4) Bunge, baada ya kutilia maanani sababu za Rais,linaweza kuupitisha Mswada huo kwa mara ya pili bila marekebisho au ukiwa na marekebisho ambayo hayakuyapa nafasi kwa kikamilifu hoja za Rais kwa kura ambayo itaungwa mkono na- (a) Thuluthi mbili ya wabunge wa Baraza la Kitaifa; na (b) Thuluthi mbili ya uwakilishi katika Seneti, iwapo ni Mswada unaohitaji idhini ya Seneti. (5) Iwapo Bunge litapitisha Mswada chini ya ibara ya (4)- (a) Spika wa Bunge husika atahitajika baada ya siku saba auwakilishe tena mswada huo kwa Rais; na (b) Rais atauwekea sahihi Mswada huo katika muda wa siku saba. (6) Iwapo Rais hatauwekea sahihi Mswada huo au kuurejesha kwa wakati unaopendekezwa katika Ibara ya (1), au au aweke sahihi chini ya ibara ya (5) (b), mswada huo utachukuliwa kama ulioidhinishwa kufikia kumalizika kwa kipindi hicho.
Soma kifungu kamili →Bunge huhakikisha wanaofanya kazi wanafanya vizuri.
(1) Uamuzi wa Baraza la Mawaziri utakuwa kwa maandishi. (2) Mawaziri wanawajibika kwa pamoja na kibinafsi kwa Rais katika kutekeleza mamlaka na utendaji wa majukumu yao. (3) Waziri atahudhuria kikao cha kamati maalumu ya Baraza la Kitaifa anapohitajika na kamati ili kujibu swali lolote kuhusu suala linalomhusu. (4) Mawaziri- (a) wataendesha shughuli za kulingana na Katiba hii; na (b) watawasilisha kwa Bunge ripoti kamili na za mara kwa mara kuhusu masuala yaliyo chini ya udhibiti wao.
Soma kifungu kamili →Watu wazima hupiga kura kuchagua viongozi wapya.
(1) Kila mwananchi ana uhuru wa kuwa na uchaguzi wa kisiasa, ikiwemo haki ya – (a) kuunda, au kushiriki katika uundaji wa chama cha kisiasa; (b) kushiriki katika shughuli za, au kusajili wanachama kwa niaba ya chama cha kisiasa; au (c) kufanyia kampeni chama cha kisiasa. (2) Kila mwananchi ana haki ya kushiriki katika uchaguzi huru, wa haki na unaofanyika mara kwa mara kwa misingi ya haki ya kupiga kura kwa wote na uhuru wa hiari ya mpiga kura kwa - (a) shirika au afisi yoyote ya umma iliyobuniwa chini ya Katiba hii na inayofanya uchaguzi; na (b) kiongozi wa afisi yoyote ya chama cha kisiasa ambacho mwananchi huyo ni mwanachama. (3) Kila raia akiwa mtu mzima ana haki pasipo na masharti yasiyo na busara,- (a) kujiandikisha kama mpiga kura; (b) kupiga kura ya siri katika uchaguzi wowote au katika kura ya maamuzi; na (c) kugombea wadhifa katika afisi ya umma, au afisi katika chama cha kisiasa ambacho yeye ni mwanachama na endapo atachaguliwa, ashike usukani.
Soma kifungu kamili →Hutahitaji kuwa kiongozi ili kushiriki.
Waambie viongozi wako kile eneo lako linahitaji.
Jifunze haki zako na uwafundishe rafiki.
Ukiwa na miaka 18, unaweza kusaidia kuchagua viongozi.
(1) Kila mwananchi ana uhuru wa kuwa na uchaguzi wa kisiasa, ikiwemo haki ya – (a) kuunda, au kushiriki katika uundaji wa chama cha kisiasa; (b) kushiriki katika shughuli za, au kusajili wanachama kwa niaba ya chama cha kisiasa; au (c) kufanyia kampeni chama cha kisiasa. (2) Kila mwananchi ana haki ya kushiriki katika uchaguzi huru, wa haki na unaofanyika mara kwa mara kwa misingi ya haki ya kupiga kura kwa wote na uhuru wa hiari ya mpiga kura kwa - (a) shirika au afisi yoyote ya umma iliyobuniwa chini ya Katiba hii na inayofanya uchaguzi; na (b) kiongozi wa afisi yoyote ya chama cha kisiasa ambacho mwananchi huyo ni mwanachama. (3) Kila raia akiwa mtu mzima ana haki pasipo na masharti yasiyo na busara,- (a) kujiandikisha kama mpiga kura; (b) kupiga kura ya siri katika uchaguzi wowote au katika kura ya maamuzi; na (c) kugombea wadhifa katika afisi ya umma, au afisi katika chama cha kisiasa ambacho yeye ni mwanachama na endapo atachaguliwa, ashike usukani.
Soma kifungu kamili →Kama kuna jambo lisilo la haki, mahakama na tume zinaweza kusaidia.
(1) Kila mtu ana haki ya kuwasilisha kesi mahakamani akidai kunyimwa, kukiukwa, au kutishiwa haki au uhuru wa kimsingi ulioko katika Sheria ya Haki (2) Pamoja na kuwasilishwa na mtu anayewawakilisha, kesi chini ya ibara ya (1) inaweza kuwasilishwa mahakamani na- (a) mtu anayemwakilisha mtu mwingine asiyeweza kujiwakilisha; (b) mtu ambaye pia ni mwanachama wa kundi fulani au kwa hiari ya kundi au tabaka fulani la watu; (c) mtu aliyejitolea kwa niaba ya umma; na (d) muungano uliojitolea kwa niaba ya mtu mmoja au kundi miongoni mwa wanachama. (3) Jaji Mkuu ataweka kanuni zinazoruhusu kesi zilizotajwa katika kifungu hiki ambazo zitaridhisha kigezo kwamba- (a) haki za kulalamika zilizotolewa katika ibara ya (2) zinatekelezwa kwa ukamilifu; (b) urasmi unaohusiana na kesi hizo, kukiwemo kuanzishwa kwa kesi, unawekwa kwa kiwango cha chini, na hasa pakiwa na haja, mahakama itakubali kuwepo kwa kesi kwa misingi ya rekodi zisizo na ulazima wa urasmi; (a) hakuna fedha zitakazotozwa kwa kuanzisha kesi; (b) mahakama, kwa kuzingatia kanuni za haki za kimsingi haitazuiwa bila sababu na mahitaji madogo madogo; na (c) shirika au mtu binafsi mwenye ujuzi maalum anaweza, kwa idhini ya mahakama, kujitokeza kama rafiki wa mahakama. (4) Kukosekana kwa kanuni zinazoangaziwa katika ibara ya (3) hakutamnyima yeyote haki ya kuwasilisha malalamiko kulingana na Kifungu hiki, kusikizwa kwa malalamiko hayo na kuamriwa na mahakama.
Soma kifungu kamili →| Wananchi | Huchagua viongozi. |
|---|---|
| Katiba | Kitabu cha sheria kwa kila mtu. |
| Bunge | Hutunga sheria. |
| Rais na serikali | Hufanya kazi. |
| Mahakama | Huhakikisha sheria zinafuatwa. |
| Gavana na Bunge la Kaunti | Huendesha kaunti yako. |
Hizi ni sheria halisi katika Katiba.
(1) Mamlaka yote makuu ni ya wananchi wa Kenya na yanaweza kutekelezwa tu kulingana na Katiba hii.
Soma kifungu kamili →(1) Katiba hii ni sheria kuu ya Jamhuri na inaunganisha asasi zote za nchi katika viwango vyote viwili vya Serikali na watu wote.
Soma kifungu kamili →(1) Eneo la Kenya limegawanywa katika kaunti zilizotajwa katika Mpangilio wa Kwanza.
Soma kifungu kamili →(2) Serikali katika viwango vya kitaifa na kaunti ni tofauti na zinategemeana na Zitaendesha mahusiano yao ya uelewanaji kwa misingi ya mashauriano na ushirikiano.
Soma kifungu kamili →(1) Mamlaka ya utungaji wa sheria ya Jamhuri hii inatokana na wananchi na katika kiwango cha kitaifa, yamekabidhiwa kwa na kutekelezwa na Bunge. (2) Bunge hufuatilia uanuwai wa taifa, huwakilisha nia ya wananchi, na hutekeleza Mamlaka yao. (3) Bunge linaweza kukubali na kupitisha marekebisho kwenye Katiba hii na kubadilisha mipaka ya kaunti kama inavyoagizwa katika Katiba hii; (4) Bunge litalinda Katiba hii na kudumisha utawala wa kidemokrasia katika Jamhuri hii. (5) Hakuna mtu yeyote au asasi yoyote, isipokuwa Bunge, itakayokuwa na mamlaka ya kuunda masharti yatakayokuwa na nguvu za kisheria nchini Kenya isipokuwa kwa amri ya Katiba hii iliyokabidhiwa Bunge au kwa Sheria ya Bunge. (6) Sheria ya Bunge, au sheria ya kaunti, inayoipatia asasi yoyote ya Serikali, afisa wa Serikali, au mtu yeyote mamlaka ya kutunga masharti au sheria na kuipatia nguvu za kisheria nchini Kenya, kama inavyokusudiwa katika Ibara ya (5), itaeleza bayana na kwa hakika shabaha na malengo ya kukabidhiwa mamlaka haya, viwango vya mamlaka, hali na upeo wa sheria zitakavyotungwa, na kanuni na viwango vya ubora vinavyotumika kisheria na vilivyobuniwa chini ya mamlaka haya.
Soma kifungu kamili →(1) Baraza la Kitaifa linawakilisha watu wa maeneobunge na walio na maslahi maalumu katika Baraza la Kitaifa. (2) Baraza la Kitaifa hushauriana kuhusu na kusuluhisha masuala yenye umuhimu mkubwa kwa watu. (3) Baraza la Kitaifa linatunga sheria kwa kuzingatia Sehemu ya 4 ya Sura hii. (4) Baraza la Kitaifa - (a) hubainisha ugavi wa mapato ya kitaifa kati ya ngazi za Serikali, kama inavyoagizwa katika Sehemu ya 4 ya Sura ya Kumi na Mbili; (b) hugawa hazina ya fedha kwa matumizi ya Serikali ya kitaifa na asasi nyingine za Serikali ya kitaifa; na (c) hutekeleza usimamizi wa jumla wa mapato ya kitaifa pamoja na matumizi yake. (5) Baraza la Kitaifa- (a) linachunguza utendakazi wa Rais afisini, Naibu wa rais na maafisa wengine wa Serikali na ikiwezekana kuchukua hatua za kuwatoa afisini; na (b) litasimamia asasi za Serikali; (6) Baraza la Kitaifa litaidhinisha tangazo la vita na kutathmini ongezeko la hali ya hatari nchini.
Soma kifungu kamili →(1) Mamlaka kuu ya Serikali yanatokana na Wakenya na yatatekelezwa kwa mujibu wa Katiba hii.
Soma kifungu kamili →(1) Rais - (a) ndiye Kiongozi wa Taifa na Serikali; (b) anatekeleza mamlaka makuu ya Jamhuri kwa usaidizi wa Naibu wa Rais na Mawaziri; (c) ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Kenya; (d) ndiye mwenyekiti wa Baraza la Kitaifa la Usalama (e) ni ishara ya umoja wa kitaifa. (2) Rais - (a) ataiheshimu, kuifuata na kuilinda Katiba; (b) ataulinda uhuru wa Jamhuri ya Kenya. (c) atakuza na kudumisha umoja wa taifa. (d) atakuza heshima ya uanuwai wa watu wa Kenya; na (e) kuhakikisha ulinzi wa uhuru na haki za kimsingi za raia na utawala wa sheria. (3) Rais hatasimamia afisi nyingine yoyote ya Serikali au ya umma.
Soma kifungu kamili →(1) Mamlaka ya Mahakama yanatokana na watu, yanajikita katika mahakama na mahakama maalum zinazobuniwa kulingana na Katiba hii. (2) Katika kutekeleza majukumu ya kimahakama, mahakama na mahakama maalum zitaongozwa na kanuni zifuatazo- (a) haki itatendwa kwa kila mtu bila kuzingatia hadhi ; (b) Haki haitacheleweshwa; (c) njia m’badala za kusuluhisha kesi zikiwemo msamaha, mashauriano, na maridhiano na njia za kitamaduni za kusuluhisha migogoro zitaimarishwa, kwa mujibu wa ibara ya (3); (d) haki itatolewa kwa kuzingatia matatizo yaliyopo ya utaratibu wa kitaalamu; na (e) lengo na kanuni za Katiba hii zitatunzwa na kuendelezwa. (3) Mbinu za kitamaduni za utatuaji wa migogoro hazitatumiwa kwa njia ambayo- (a) itakiuka Sheria za Haki; (b) itagongana na haki na maadili au kusababisha matokeo yatakayogongana na haki na maadili; (c) haiambatani na Katiba hii au sheria yoyote iliyoandikwa.
Soma kifungu kamili →(1) Katika utekelezaji wa mamlaka ya mahakama, Mahakama kama ilivyoundwa chini ya kifungu cha 161, itazingatia Katiba hii pamoja na sheria na haitadhibitiwa wala kuelekezwa na mtu yeyote mwingine au halmashauri. (2) Afisi ya jaji wa mahakama ya Mamlaka Kuu haitafutiliwa mbali wakati ambapo kuna afisa anayeshikilia wadhifa huo. (3) Mishahara na marupurupu yanayofaa kulipwa, au kuhusiana na, majaji yatatoka kwa Mfuko wa Jumla wa Serikali. (4) Kulingana na Kifungu cha 168 (6), mishahara na marupurupu inayofaa kulipwa, au kuhusiana na majaji haitabadilishwa kwa njia itakayowaathiri, na marupurupu ya kustaafu ya jaji hayatabadilishwa ili kumuathiri jaji mstaafu katika maisha yake ya uhai. (5) Mwanachama wa mahakama hatawajibika katika hatua au kesi kuhusiana na chochote watakachofanya au watakachokosa kufanya kwa nia njema katika utendaji kazi wa kisheria kwa kutekeleza majukumu ya mahakama.
Soma kifungu kamili →Malengo ya Serikali ya ugatuzi ni- (a) kuhakikisha kuwa kuna mamlaka ya kidemokrasia na uwajibikiaji wa Serikali ; (b) kuhimiza umoja wa kitaifa kwa kutambua uanuwai wa jamii mbalimbali; (c) kuwapa watu katika kila ngazi mamlaka ya kujitawala na kushiriki katika matumizi ya mamlaka ya Serikali katika kufanya maamuzi ya mambo yanyowaathiri; (d) kutambua haki za jamii zote katika kusimamia masuala ya jamii zao na kujiendeleza zaidi; (e) kulinda na kuhamasisha maslahi na haki za jamii za watu walio wachache na zile za watu waliotengwa; (f) kustawisha miradi ya kijamii na kiuchumi na utoaji wa huduma za karibu na zilizo rahisi ili kumfikia kila mtu nchini Kenya; (g) kuhakikisha kuna ugavi sawa wa rasilmali zote za kijamii na za kitaifa kote nchini. (h) kufanikisha ugatuzi wa mamlaka ya taasisi za Serikali, uendeshaji wake wa shughuli ama huduma kutoka mji mkuu wa Kenya; na (i) kuhakikisha kuna kudhibiti na kugawana mamlaka kwa njia iliyo sawa.
Soma kifungu kamili →(1) Katika kipindi cha muda wa siku kumi na nne baada ya kupokea Mswada, Rais- (a) ataweka saini; au (b) ataurejesha Mswada Bungeni ili kuchunguzwa upya na Bunge huku likitilia maanani sababu alizo nazo Rais za kutouidhinisha mswada huo. (2) Iwapo Rais ataurejesha Mswada bungeni kuchunguzwa upya, Bunge kwa kuzingatia taratibu zinazofaa kama zilivyotajwa katika sehemu hii, linaweza- (a) kuurekebisha Mswada huo kwa kuangazia sababu muhimu alizotoa Rais; au (b) kuupitisha Mswada huo kwa mara ya pili bila kufanya marekebisho. (3) Iwapo Bunge limerekebisha Mswada huo huku likitilia maanani kikamilifu hoja za Rais, Spika anayehusika atampelekea Rais tena ili aweke sahihi. (4) Bunge, baada ya kutilia maanani sababu za Rais,linaweza kuupitisha Mswada huo kwa mara ya pili bila marekebisho au ukiwa na marekebisho ambayo hayakuyapa nafasi kwa kikamilifu hoja za Rais kwa kura ambayo itaungwa mkono na- (a) Thuluthi mbili ya wabunge wa Baraza la Kitaifa; na (b) Thuluthi mbili ya uwakilishi katika Seneti, iwapo ni Mswada unaohitaji idhini ya Seneti. (5) Iwapo Bunge litapitisha Mswada chini ya ibara ya (4)- (a) Spika wa Bunge husika atahitajika baada ya siku saba auwakilishe tena mswada huo kwa Rais; na (b) Rais atauwekea sahihi Mswada huo katika muda wa siku saba. (6) Iwapo Rais hatauwekea sahihi Mswada huo au kuurejesha kwa wakati unaopendekezwa katika Ibara ya (1), au au aweke sahihi chini ya ibara ya (5) (b), mswada huo utachukuliwa kama ulioidhinishwa kufikia kumalizika kwa kipindi hicho.
Soma kifungu kamili →(1) Uamuzi wa Baraza la Mawaziri utakuwa kwa maandishi. (2) Mawaziri wanawajibika kwa pamoja na kibinafsi kwa Rais katika kutekeleza mamlaka na utendaji wa majukumu yao. (3) Waziri atahudhuria kikao cha kamati maalumu ya Baraza la Kitaifa anapohitajika na kamati ili kujibu swali lolote kuhusu suala linalomhusu. (4) Mawaziri- (a) wataendesha shughuli za kulingana na Katiba hii; na (b) watawasilisha kwa Bunge ripoti kamili na za mara kwa mara kuhusu masuala yaliyo chini ya udhibiti wao.
Soma kifungu kamili →(1) Kila mwananchi ana uhuru wa kuwa na uchaguzi wa kisiasa, ikiwemo haki ya – (a) kuunda, au kushiriki katika uundaji wa chama cha kisiasa; (b) kushiriki katika shughuli za, au kusajili wanachama kwa niaba ya chama cha kisiasa; au (c) kufanyia kampeni chama cha kisiasa. (2) Kila mwananchi ana haki ya kushiriki katika uchaguzi huru, wa haki na unaofanyika mara kwa mara kwa misingi ya haki ya kupiga kura kwa wote na uhuru wa hiari ya mpiga kura kwa - (a) shirika au afisi yoyote ya umma iliyobuniwa chini ya Katiba hii na inayofanya uchaguzi; na (b) kiongozi wa afisi yoyote ya chama cha kisiasa ambacho mwananchi huyo ni mwanachama. (3) Kila raia akiwa mtu mzima ana haki pasipo na masharti yasiyo na busara,- (a) kujiandikisha kama mpiga kura; (b) kupiga kura ya siri katika uchaguzi wowote au katika kura ya maamuzi; na (c) kugombea wadhifa katika afisi ya umma, au afisi katika chama cha kisiasa ambacho yeye ni mwanachama na endapo atachaguliwa, ashike usukani.
Soma kifungu kamili →(1) Kila mtu ana haki ya kuwasilisha kesi mahakamani akidai kunyimwa, kukiukwa, au kutishiwa haki au uhuru wa kimsingi ulioko katika Sheria ya Haki (2) Pamoja na kuwasilishwa na mtu anayewawakilisha, kesi chini ya ibara ya (1) inaweza kuwasilishwa mahakamani na- (a) mtu anayemwakilisha mtu mwingine asiyeweza kujiwakilisha; (b) mtu ambaye pia ni mwanachama wa kundi fulani au kwa hiari ya kundi au tabaka fulani la watu; (c) mtu aliyejitolea kwa niaba ya umma; na (d) muungano uliojitolea kwa niaba ya mtu mmoja au kundi miongoni mwa wanachama. (3) Jaji Mkuu ataweka kanuni zinazoruhusu kesi zilizotajwa katika kifungu hiki ambazo zitaridhisha kigezo kwamba- (a) haki za kulalamika zilizotolewa katika ibara ya (2) zinatekelezwa kwa ukamilifu; (b) urasmi unaohusiana na kesi hizo, kukiwemo kuanzishwa kwa kesi, unawekwa kwa kiwango cha chini, na hasa pakiwa na haja, mahakama itakubali kuwepo kwa kesi kwa misingi ya rekodi zisizo na ulazima wa urasmi; (a) hakuna fedha zitakazotozwa kwa kuanzisha kesi; (b) mahakama, kwa kuzingatia kanuni za haki za kimsingi haitazuiwa bila sababu na mahitaji madogo madogo; na (c) shirika au mtu binafsi mwenye ujuzi maalum anaweza, kwa idhini ya mahakama, kujitokeza kama rafiki wa mahakama. (4) Kukosekana kwa kanuni zinazoangaziwa katika ibara ya (3) hakutamnyima yeyote haki ya kuwasilisha malalamiko kulingana na Kifungu hiki, kusikizwa kwa malalamiko hayo na kuamriwa na mahakama.
Soma kifungu kamili →